KILICHOJIRI LEO MLIMANI TV, KWENYE MAHOJIANO NA SHAMIRA MSHANGAMA

Mgombea nafasi ya Umakamu wa Rais wa DARUSO, Shamira Mshangama, akiwa kwenye kipindi cha Mahojiano ya moja kwa Moja na Mlimani TV, kwenye kipindi cha Mlimani Leo kinachorushwa kila siku kuanzia saa 1 kamili mpaka saa 3 kamili asubuhi.


Mgombea Nafasi ya Umakamu wa Urais wa DARUSO, Shamira Mshangama akieleza jambo wakati wa mahojiano ya moja kwa moja na Silvano Kayela ndani ya Mlimani TV leo asubuhi kwenye kipindi cha Mlimani Leo.Akijibu swali alililoulizwa na Msimamizi wa kipindi hicho Bwana Silvano kayela, Shamira amesema kuwa aligombea nafasi hiyo na si ya Urais kwa sababu ya Mfumo dume uliokithiri miongoni mwa wanajamii.
Na kutumia fursa hiyo kuwaomba wanaudsm wampe kura za kutosha ili akawatumikie wanaudsm, kama Moto wake unavyosema MIMI NI MTUMWA WENU NITUMENI.

                          (PICHA ZOTE NA MUNIRA HUSSEIN)

WANGOFIRA BLOG INAWATAKIA WAGOMBEA WOTE KILA LA KHERI KWENYE UCHAGUZI MKUU WA DARUSO UTAKAO FANYIKA SIKU YA JUMATATU YA TAR 2 MEI, 2016.

PIA BLOG HII INAOMBA RADHI KWA KUELEKA VIBAYA NA BAADHI YA WANAUDSM KUWA INAENDESHWA KWA USHABIKI WA WAGOMBEA FULANI.

NAENDELEA KUSISITIZA, KUWA BLOG HII IKO HURU NA HAIFANYI KAZI KWA MASLAHI YA BAADHI YA WAGOMBEA.

AKSANTENI.
KILICHOJIRI LEO MLIMANI TV, KWENYE MAHOJIANO NA SHAMIRA MSHANGAMA KILICHOJIRI LEO MLIMANI TV, KWENYE MAHOJIANO NA SHAMIRA MSHANGAMA Reviewed by Unknown on 00:06:00 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.