Jukwaa La Wahariri Lalitaka Bunge Kuacha Kufunika Shughuli za Bunge Kwenye Blanketi Zito La Usiri

 

Jukwaa la la wahariri nchini Tanzania TEF imetoa rai kwa uongozi wa Bunge kufikiria upya hatua za kuzidi kufunika shughuli za Bunge kwenye Blanketi zito la usiri na badala yake uruhusu kituo chochote cha televisheni chenye nia,uwezo na utayari wa kurusha Matangazo ya Bunge moja kwa moja bila kulazimisha kujiunga na FEED Maalumu iliyoanzishwa . 
 
 Akitoa tamko hilo Mwenyekiti wa Jukwa la Wahariri Theophil Makunga amesema habari kutoka ndani ya bunge sasa zinachujwa mno kupitia mfumo huu mpya wa FEED Maalamu. 
 
 Aidha Mwenyekiti huyo wa TEF amesema ubora wa picha zinazorushwa kupitia FEED hii nao ni wa kiwango cha chini pia. 
 
Wakati Deodatus Balile amesema hatua itakayofuata ni wajumbe wa TEF kuelekea Bungeni kwa ajili ya kuzugumza swala hilo kwani inawanyima wananchi haki ya kuipata kwa uhakika na bila kuchujwa kile ikinachofanywa na wawakilishi wao.

Jukwaa La Wahariri Lalitaka Bunge Kuacha Kufunika Shughuli za Bunge Kwenye Blanketi Zito La Usiri Jukwaa La Wahariri Lalitaka Bunge Kuacha Kufunika Shughuli za Bunge Kwenye Blanketi Zito La Usiri Reviewed by WANGOFIRA on 21:25:00 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.