VYUO VYA AFYA VITAKAVYOCHUKUA WANAFUNZI APRIL 2016

BARAZA LA TAIFA LA ELIMU YA UFUNDI

    

MAOMBI YA NAFASI ZA MAFUNZO MWAKA WA MASOMO MACHI 2016/2017

Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa kushirikiana na Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) wanatangaza nafasi za masomo kwa kozi mbalimbali za afya zinazotolewa na vyuo vilivyosajiliwa na NACTE na kutambuliwa na wizara. Vyuo vitakavyoendesha mafunzo haya kwa muda huu ni:

BONYEZA HAPA KUONA VYUO HIVYO 
  Muda wa Mafunzo:  
  • Miaka mitatu (3)kwa kozi za Stashahada (Ordinary Diploma)
  • Miaka miwili (2) kwa kozi za astashahada (Technician Certificate)
  • Mwaka mmoja (1) kwa astashahada ya awali (Basic Technician Certificate)
  1. Sifa za Muombaji Watarajali (Pre-service):
  2. Kozi za stashahada (ordinary diploma)
  • Kozi za Stashahada ya Maabara (Ordinary Diploma in medical laboratory sciences) amemaliza kidato cha nne na ufaulu wake  uwe wa kiwango kisichopungua alama ya ‘C’,  kwa masomo ya biologia na kemia , na alama ‘D’ kwa somo la fizikia, Hisabati na Kingereza kwa  .
  • kozi za Stashahada ya uuguzi na ukunga (ordinary diploma in nursing and midwifery)Awe amemaliza kidato cha nne  na ufaulu wake  uwe wa kiwango kisichopungua alama ya ‘C’,  kwa masomo ya biologia na kemia , na alama ‘D’ kwa somo la fizikia. ufaulu wa  Hisabati na Kingereza ni sifa ya ziada
  • kozi za Stashahada ya Utabibu (ordinary diploma in clinical Medicine)Awe amemaliza kidato cha nne  na ufaulu wake  uwe wa kiwango kisichopungua alama ya ‘C’,  kwa masomo ya biologia na kemia , na alama ‘D’ kwa somo la fizikia. ufaulu wa  Hisabati na Kingereza ni sifa ya ziada

  • Kozi za astashahada (technician certificates)
  • Astashahada ya  maabara (Technician Certificate medical laboratory sciences).  amemaliza kidato cha nne  na ufaulu wake  uwe wa kiwango kisichopungua alama ‘D’, kwa masomo ya biologia, Kemia, Fizikia, Hisabati na Kiingereza.
  • Astashahada ya Uuguzi na ukunga (Technician Certificate nursing and midwifery). awe amemaliza kidato cha nne  na ufaulu wake  uwe wa kiwango kisichopungua alama ‘D’, kwa masomo ya biologia, Kemia, Fizikia.  Hisabati na Kiingereza ni sifa za ziada
  • Astashahada ya Utabibu  (Technician Certificate clinical medicine). awe amemaliza kidato cha nne  na ufaulu wake  uwe wa kiwango kisichopungua alama ‘D’, kwa masomo ya biologia, Kemia, Fizikia.  Hisabati na Kiingereza ni sifa za ziada
  1. Astashahada ya awali (basic Technician certificate)
  • Uhudumu wa afya (Community Health worker) awe memaliza kidato cha nne  na ufaulu wake  uwe wa kiwango kisichopungua alama ‘D’, kwa masomo manne (4), somo la biolojia (Biology) likiwa nilazima  
  • Watoaji dawa muhimu (Dispencers) awe amemaliza kidato cha nne  na ufaulu wake  uwe wa kiwango kisichopungua alama ‘D’, kwa masomo manne (4), somo la biolojia (Biology) likiwa ni lazima.
  1. Utaratibu wa kutuma maombi:Maombi yatafanyika kwa  njia ya mtandao kupitia mfumo wa udahiri wa pamoja (Central Admission System-CAS) unaoendeshwa na kusimamiwa na NACTE.Aidha mfumo huu unapatikana kupitia Tovuti: www.nacte.go.tz  au  www.cas.go.tz 
  2. Utaratibu wa kutoa taarifa kwa waliochaguliwa:
  3. Baraza la Elimu ya Ufundi (NACTE) litakuwa na wajibu wa kuwataarifu wale wote watakaofanikiwa kuchaguliwa kujiunga na kozi mbalimbali kupitia ‘website’ ya Baraza na pia kupitia utaratibu mwingine wowote utakaodhihirika kurahisisha mawasiliano na utoaji taarifa.
  4. Taarifa hizo zitatumwa pia vyuoni kwa ajili ya ufatiliaji na urahisishaji wa mawasiliano.
  5. Muda wa mwisho wa kuomba kujiunga ni tarehe 31 Marchi, 2016.
  6. Muhula wa masomo unatarajiwa kuanza tarehe 18 April, 2016.
Imetolewa na:
Kaimu Katibu Mtendaji,
Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi
S.L.P. 7109,
Dar es Salaam
VYUO VYA AFYA VITAKAVYOCHUKUA WANAFUNZI APRIL 2016  VYUO VYA AFYA VITAKAVYOCHUKUA WANAFUNZI APRIL 2016 Reviewed by WANGOFIRA on 21:57:00 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.