UKWELI KUHUSU AJIRA MPYA ZA WALIMU 2016.


KUNA  TAARIFA ZINAENEA KWA KASI MITANDAONI KUHUSU SERIKALI KUTO KUWAPOKEA WASOMI WENYE CHETI ZAIDI YA KIMOJA KATIKA AJIRA..UJUMBE WENYEWE UNAMUHUSISHA WAZIRI SIMBACHAWENE NA UKISOMEKA HIVI:-

Waziri Simbachawene ametoa tamko la serikali kuwa , Serikali ya Jamhuri Ya Muungano wa Tanzania haiko tayari kuajiri wasomi wenye vyeti vya baraza la mitihani kuanzia vyeti viwili na kuendelea,watakaopata ajira yoyote ile ya moja kwa moja serikalini ni wasomi wenye cheti kimoja tu. Wale waliosoma kwa kuunga unga, mara kutafuta credit, mara kurudia mitihani watafute ajira kwa mashirika binafsi.Serikali inataka kuwaajiri wasomi wenye cheti kimoja tu waliosoma moja kwa moja. System hii itaanza kwenye ajira za walimu za mwaka huu 2016 zinazoenda kutangazwa mda si mrefu mwezi wa nne mwanzoni. Simbachawene ameyasema hayo akiwa na waandishi wa habari jijini Dar leo majira ya asubuhi ili kuwajuza watanzania kuwa ni tamko la serikali.
Rai kwa wenye vyeti vingi, mtakua mnaomba ajira kivyenu serikalini au kwa mashirika binafsi na si kuajiliwa moja kwa moja kutoka serikali kama ilivyokua awali.
Samahani kwa usumbufu uliojitokeza.
Imetolewa na Afsa mawasiliano, wa Tamisemi.

Ndg.Elnest kimash
Dar es salaam.
UKWELI KUHUSU AJIRA MPYA ZA WALIMU 2016. UKWELI KUHUSU AJIRA MPYA ZA WALIMU 2016. Reviewed by WANGOFIRA on 21:26:00 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.