MWANAFUNZI WA KIDATO CHA SITA THAQAAFA ACHINJWA AKIWA KWENYE KILABU CHA POMBE.


Mwanafunzi wa kidato cha sita wa Shule ya Sekondari Thaqaafa ya jijini Mwanza, Amos Kitala (26) ameuawa kwa kuchinjwa kwa kipande cha chupa shingoni kwenye kilabu cha pombe za kienyeji. 
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Justus Kamugisha alisema tukio hilo lilitokea Machi 19, mwaka huu saa 10 jioni wakati mwanafunzi huyo akigombana na watu wawili kwenye kilabu hicho. 
Kamugisha alisema inadaiwa kabla ya kuuawa Kitala alionekana kuwazidi nguvu wagomvi wake na ndipo walipoamua kuchukua chupa, kuivunja na kumkata nayo shingoni na kusababisha atokwe damu nyingi. Kamgisha alisema wanamshikilia Ramadhan Sima (27) na Omary Philipo (35) kwa tuhuma za mauaji hayo. 
MWANAFUNZI WA KIDATO CHA SITA THAQAAFA ACHINJWA AKIWA KWENYE KILABU CHA POMBE. MWANAFUNZI WA KIDATO CHA SITA THAQAAFA ACHINJWA AKIWA KWENYE KILABU CHA POMBE. Reviewed by Unknown on 11:23:00 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.