MKURUGENZI AFARIKI DUNIA GHAFLA, SIKU MOJA KABLA MAJALIWA KUFIKA WILAYANI HUMO KWA ZIARA


Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Maswa mkoani Simiyu, Trasius Kagenzi amefariki dunia ghafla kutokana na shinikizo la damu. Picha ya Maktaba. 
Maswa. Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Maswa mkoani Simiyu, Trasius Kagenzi amefariki dunia ghafla kutokana na shinikizo la damu.
Habari zilizopatikana kutoka Maswa zilisema jana kuwa Kagenzi alifariki dunia saa nane usiku wa kuamkia jana katika Hospitali ya Rufaa Bugando alikohamishiwa kutoka Hospitali ya Wilaya Maswa.
Kagenzi aliyewahi kuwa DED wa Tarime, Igunga na Arumeru alipata shinikizo la damu juzi wakati akifanya mazoezi na kushindwa kuendelea, ndipo alipopelekwa katika hospitali ya wilaya na kupewa rufaa kwenda Bugando.
Kifo hicho kimetokea siku moja kabla ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa aliyeko ziarani mkoani Simiyu kutembelea wilaya hiyo leo.
Katibu Tawala msaidizi Mkoa wa Simiyu, Simon Maganga alisema kifo hicho kimeacha pengo kubwa hasa kwa kuzingatia kuwa kwa miaka miwili aliyokaa Maswa, Kagenzi alifanikiwa kuwanganisha watumishi waliokuwa hawaelewani na halmashauri ilikuwa inasonga mbele.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Maswa, Godfrey Machumu alisema Kagenzi ameondoka wakati anahitajika sana kutokana na kutokamilika kwa mipango ambayo wakurugenzi wa wilaya za Mkoa wa Simiyu walikuwa wameweka kuendeleza mkoa huo.
CHANZO; MWANANCHI

//
MKURUGENZI AFARIKI DUNIA GHAFLA, SIKU MOJA KABLA MAJALIWA KUFIKA WILAYANI HUMO KWA ZIARA MKURUGENZI AFARIKI DUNIA GHAFLA, SIKU MOJA KABLA MAJALIWA KUFIKA WILAYANI HUMO KWA ZIARA Reviewed by Unknown on 01:20:00 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.