MAGUFULI ALA CHAKULA MCHAHAWANI MWANZA

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Joseph Pombe Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli pamoja na viongozi wa mkoa wa Mwanza wakijipatia chakula cha mchana katika mgahawa wa Victoria uliopo nje ya Uwanja wa Ndege wa Mwanza alipopumzika kwa muda kabla ya kuelekea nyumbani kwake Chato mkoani Geita kwa mapumziko mafupi.


Pamoja nao mezani hapo ni Meya wa Ilemela Mstahiki Renatus Mulunga, Meya wa jiji la Mwanza Mstahiki James Bwire, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe John Mongella na Mwenyekiti wa CCM Mkoa huo Ndg Anthony Diallo. 
 
 
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Joseph Pombe Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli pamoja na viongozi wa mkoa wa Mwanza wakiondoka baada ya kupata chakula cha mchana katika mgahawa wa Victoria uliopo nye ya Uwanja wa Ndege wa Mwanza alipopumzika kwa muda kabla ya kuelekea nyumbani kwake Chato mkoani Geita kwa mapumziko mafupi. 
MAGUFULI ALA CHAKULA MCHAHAWANI MWANZA MAGUFULI ALA CHAKULA MCHAHAWANI MWANZA Reviewed by WANGOFIRA on 21:29:00 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.