RAIS UHURU KENYATA WA KENYA ASHIRIKI UZINDUZI WA OFISI ZA UNION KONFERENSI YA KANISA LA SDA NCHINI KENYA

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta ameshiriki na viongozi wa Kanisa la Waadventista Wa Sabato katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati kwenye uzinduzi wa ofisi za Unioni Konferensi ya Magharibi mwa Kenya.

 Kwenye uzinduzi huo uliofanyika  Kisumu ulihudhuriwa na viongozi wandamizi wa ECD wakiongozwa na mwenyekiti wa ECD,  Dr Blasious Ruguri. Mbali na hayo  Rais Kenyata amelipongeza kanisa la Waadventista Wa Sabato kwa namna linavyojishughulisha katika kutatua matatizo ya jamii hasa kwa vijana na kuahidi ushirikiano mkubwa kutoka serikani  kwa kanisa hilo katika kusogeza mbele maendeleo katika jamii ambapo alichangia sh.milioni 2 za Kenya kwa ajili ya vyombo vya habari katika Unioni Konferensi hiyo.




Rais Uhuru Kenyata hakiutubia mamia ya watu waliohudhulia kwenye uzinduzi huo (hawapo pichani)




Rais Kenyata akiwasili viwanjani tayari kwa shughuli ya Uzinduzi


Rais Kenyatta akisalimiana na mwenyekiti wa ECD, DR. Ruguri



Rais Kenyatta akipanda Mti wa kumbukumbu



Rais Kenyatta akifuatilia kwa makini maonyesho ya vijana wa PathFinder ( hawapo pichani)

RAIS UHURU KENYATA WA KENYA ASHIRIKI UZINDUZI WA OFISI ZA UNION KONFERENSI YA KANISA LA SDA NCHINI KENYA RAIS UHURU KENYATA WA KENYA ASHIRIKI UZINDUZI WA OFISI ZA UNION KONFERENSI YA KANISA LA SDA NCHINI KENYA Reviewed by WANGOFIRA on 07:37:00 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.