BREAKING NEWS; TAARIFA KUHUSU FORM FOUR RESULTS

TAARIFA RASMI KUHUSU MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2015


Baraza la Mitihani la Tanzania limekuwa likipigiwa simu na watu mbalimbali wakiomba ufafanuzi kuhusu taarifa zinazosambazwakwenye mitandao ya kijamii kuwa Wizara ya Elimu, Sayansi,Teknolojia na Ufundi imetangaza kuwa matokeo ya Mtihani wa Kidato cha Nne (CSEE) 2015yamezuiwa kwa muda hadi tarehe 08/03/2016 

Baraza la Mitihani la Tanzanialinapenda kuwajulisha watahiniwa na umma kwa ujumla kuwa taarifa hizo ni za UONGO na zinalenga kupotosha umma na kuleta taharuki. 

Hivyo,Baraza linaomba umma kuzipuuza taarifa hizo kwa kuwa Wizara haijasitisha utoaji wa matokeo hayo. 


Matokeo yatatangazwa mara tu mchakato Utakapokamilika 

Imetolewa na, 

AFISA HABARI NA UHUSIANO

BREAKING NEWS; TAARIFA KUHUSU FORM FOUR RESULTS BREAKING NEWS; TAARIFA KUHUSU FORM FOUR RESULTS Reviewed by Unknown on 11:37:00 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.