Weusi 2 wapigwa risasi na kuuawa huko chicago



Afisa mmoja wa polisi amewapiga risasi watu wawili weusi alipoitwa kuchunguza kisa cha ugomvi wa kinyumbani katika mji wa West Side Chicago nchini Marekani.
Waathirika walikuwa ni Quintonio Legrier, mwanamume mwenye umri wa miaka 19 na Bettie Jones, mwanamke mwenye umri wa miaka 55.
Wote wawili walikuwa weusi, huku familia zao zikilaumu idara ya polisi kwa kutumia nguivu kupita kiasi.
Msemaji wa polisi amesema kuwa kisa hicho cha kupigwa risasi kilifanyika baada ya maofisa walipokabiliwa na kile alichokitaja kuwa kushambulizi

Mamake mtu huyo anasema kuwa mwanawe hakuwa na bunduki alipopigwa risasi.
Naye mwanaye bi Jones anadai mamake alipigwa risasi punde tu alipofungua mlango uliokuwa unabishwa kwa nguvu na afisa huyo.
Polisi mjini Chicago wamelaumiwa kwa visa vya ubaguzi na mauaji yanayoegemea misingi ya ubaguzi wa rangi.
Mapema juma lililopita wenyeji wa mji huo waliandamana kupinga mauaji ya kijana mwengine mweusi aliyepigwa risasi 16 na afisa wa polisi mzungu.
Kisa hicho kiliibua hasira miongoni mwa wenyeji.
Weusi 2 wapigwa risasi na kuuawa huko chicago Weusi 2 wapigwa risasi na kuuawa huko chicago Reviewed by WANGOFIRA on 09:09:00 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.