USWIZI YAAPA KUENDELEZA USHIRIKIANO NA TANZANIA

taarifa kwa vyombo vya habari
THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
Telegrams : "CABINET"
DAR ES SALAAM
Telephone : 2116898, 2116900/6
Fax : 2113425/2116914/2117272
PRESIDENT’S OFFICE,
THE STATE HOUSE,
1 BARACK OBAMA ROAD
11400 DAR ES SALAAM.
Uswis iimeahidi kuendeleza ushirikiano na Tanzania katika Nyanja mbalimbali za maendeleo huku mkazo mkubwa ukiuelekeza katika kuendeleza elimu ya mafunzo ya ufundi stadi.
Balozi wa Uswisi hapa Nchini Mheshimiwa Florence Tinguelly Mattli, amesema hayo leo tarehe 23 Desemba, 2015 alipokutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John PombeMagufuli Ikulu Jijini  Dar es salaam.
Balozi Florence amemueleza Rais Magufuli kuwa pamoja na kuwepo kwa miradi mingine ambayo nchi hiyo inaendelea kuitekeleza kwa kushirikiana na Tanzania, katika awamu hii Uswisi itatilia mkazo katika elimu ya ufundi stadi ilikuwawezesha vijana wanaosoma kuwa na ujuzi unaowawezesha kuzalisha bidhaa na kujipatia kipato kama ambavyo nchi ya Uswisi inafanya.
Maeneo mengin eambayo viongozi hao wamezungumzia nikuimarisha ushirikiano katika uwekezaji, ambapo Rais Magufuli amewaalika wa wekezaji kutoka Uswisi kufanya biashara na Tanzania, kuimarisha huduma za bandari na pia kuongeza uwezo katika kukabilia na na vitendo vya Rushwa.
Kuhusu Sekta ya afya, Rais Magufuli ameipongeza Uswisi kwa kushirikiana na Tanzania kupitia Taasisi yaAfya Ifakara katika kukabiliana na changamoto mbalimbali za kiafya ikiwemo kukabiliana na ugonjwa wa Malaria naameahidi kuwa Serikali itaendelea kuitumia taasisi hiyo ilikusaidiajuhudi za kukabiliananamagonjwa.
Wakati Huo Huo, Rais wa Jamhuri ya Muunganowa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amekuta na nakufanya mazungumzo na Baloziwa Kuwait hapa Nchini Mheshimiwa Jasem Al Najem Ikulu, Jijini Dar es salaam.
Katika Mazungumzo hayo, Balozi Al Najem amewasilisha salamu za mfalme  wa Kuwait Mheshimiwa Sabah Al Ahamad Al Jaber al Sabahkwa Rais Magufuli, ambaye  amempongeza kwa kuchaguliwa kuwa Rais waawamu ya tano na amemhakikishia kuwa Kuwait itaendelea kushirikian ana Tanzania katika maendeleo ikiwemo kufadhi liutekelezaji wamiradi mbalimbali katika sekta za ujenzi, Majina Kilimo.
Miongoni mwa miradi hiyo ni mradi wa ujenziC wa barabara ya Chaya – Nyahua yenye urefu wakilometa 85 kwa kiwango cha lami ambapo Tanzania imeomba ufadhili wa dola milioni 85, Mradi wa Maji wa Same - Mwanga – Korogwe ambapo Tanzania imeomba ufadhili wa dola milioni 20 na Mradi mkubwa wa kilimo cha umwagiliaji katika bonde la Mhongo na Luhiche Mkoani Kigoma ambapo Kuwait imeonesha nia ya kuufadhili.
Aidha, Rais Magufuli amemshukuru Mfalme wa Kuwait kwa salamu zake za pongezi na amewaalika wafanyabiashara wa Kuwait kushirikiana na Tanzania katika biashara na uwekezaji.
Katika Hatua nyingine Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amekutana na Waziri wa Mambo ya Njewa Rwanda Mheshimiwa Louise Mushikiwabo aliye tumwa kuleta ujumbe maalum wa Rais Paul Kagame wa Rwanda.
Katika Ujumbe huo, Mheshimiwa Kagame amemuhakikishia Rais Magufuli kuwa Rwanda itaendelea kushirikiana na Tanzania katika Nyanja mbalimbali za kiuchumi, kisiasa na kijamii hasa ikizingatiwa kuwa licha kuwa ni nchi jirani ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, Rwanda ni marafiki na ndugu wa Tanzania.
Rais Kagame pia amempongeza Rais Magufuli kwa uongozi mzuri aliounesha katika siku za mwanzo za uongozi wake wa awamu ya tano ambao amesema anauunga mkono.
Pamoja na kupokea salamu za Rais Kagame, Rais Magufuli na Waziri wa Mambo ya Nje wa Rwanda wamezungumzia mgogoro wa kisiasa unaoendelea nchini Burundi na wote kwa pamoja wameona nimuhimu kupata suluhisho kwa njia ya mazungumzo ili wananchi waweze kuishi kwa amani na kuendelea na shughuli zao za maendeleo

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es salaam
23 Desemba, 2015
USWIZI YAAPA KUENDELEZA USHIRIKIANO NA TANZANIA USWIZI YAAPA KUENDELEZA USHIRIKIANO NA TANZANIA Reviewed by WANGOFIRA on 00:56:00 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.