USHAURI WANGU KWA NAPE, WAZIRI WA HABARI, MICHEZO NA UTAMADUNI.



Na Shaaban Maulidi.Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye  akizungumza na Wakurugenzi na Viongozi wa Idara mbali mbali walio chini  ya Wizara yake ambapo aliwaambia kuwa atashirikiana nao katika kufanikisha yale yatakayowezesha tasnia ya habari, michezo , utamaduni na sanaa na sanaa kukua

(waziri wa habari, michezo, utamaduni na wasanii NAPE NAUYE, picha kwa hisani ya ADAM MZEE).

Nipende kuchukua fursa hii kumshukuru Mwenyezi Mungu ambaye amejaalia sifa njema pamoja na nguvu za kaandaa makala hii.Nachukua fursa hii pia kumpongeza Mh Nape Nnauye kwa kuteuliwa kuwa waziri wa Habari, Utamaduni, wasanii na michezo siku ya Alhamis tarehe 11 Disemba. Hii ni kutokana na ukweli kwamba Mh Rais Dkt John Magufuli amerizishwa na hali ya utendaji kazi wako na pia amekuamini. Mimi binafsi nasema "kama ni ngoma imepata mchezaji" yaani nabariki uteuzi wako ambao ulikamilika baada ya kula kiapo cha utii mbele ya Mh Rais siku ya Jumamosi Tarehe 13 Disemba ya mwaka huu. Kwani naamini wewe ni mtu makini na mchapakazi ambaye unaendana na dhana ya "HAPA KAZI TU # Kama ilivyonadiwa na Mh Rais wakati wa kampeni na kudhihirishwa kwa wananchi baada ya kuapishwa kwa Mh Rais.

Ni matumaini yangu kuwa unafahamu sehemu husika uliyeteuliwa pamoja na changamoto zinazoikabili wizara husika hususani katika nyanja ya michezo. Leo naomba nitumie nafasi hii kuelezea hisia na matarajio ya watanzania walio wengi kuhusu suala la Michezo mathalani kwa walio wapenzi wa sekta hii.

Nchi yetu ya Tanzania inakabiliwa na Changamoto kubwa katika sekta ya michezo na changamoto hizo zinaanzia katika ngazi ya utawala hapa namaanisha uongozi mbovu katika sekta ya michezo, uongozi unaojali maslahi ya mtu mmoja mmoja, bila ya kujali mafanikio ya taifa.

Uongozi uliojaa urasimu, kujuana kwingi, maslahi ya mtu mbele, mipango mibovu, na hatimaye kuliingiza Taifa katika aibu ambayo haiwezi kuvumilika hususani kwa watanzania wanahitaji mabadiliko ya kweli kwani hata sekta hii inahitaji mabadiliko. Na msimamizi wa mabadiliko haya ni wewe huku ukiungwa mkono na watanzania wengine wenye uchu wa kuiona Tanzania iking'ara katika duru ya michezo nikiwemo mimi mwenyewe.

Ukiachilia mbali suala la Uongozi, kuna hili la maeneo hasa ambapo michezo hii itafanyikia hapa namaanisha miundombinu hususani viwanja. Nchi yetu Tanzania inakabiliwa na tatizo kubwa la ukosefu wa viwanja stahiki vya kisasa ambavyo vingesaidia kutoa ari kwa vijana kuweza kushiriki vyema katika michezo kwa ajili ya kuliletea Taifa letu heshima. Suala hili limekuwa kinyume Kutokana na ukweli kwamba Tanzania hakuna viwanja vya kisasa na vinavyotakiwa kwa ajili ya kuwanoa vijana ili wakapambane kwa ajili ya Taifa Lao.

 Vingi vya viwanja vilivyo nchini ni vibovu, vya kizamani, havina mvuto, havifai kwa kujifunzia wala hata kuchezea. Lakini afadhali ya hili pia kuna uhaba wa viwanja kwa michezo ya aina yote kwani iliyopo ni michache na haiwezi kukimu haja za watanzania wote wenye mahaba na michezo, hapa si katika soka, mpira wa kikapu, riadha, mbio za magali, n. k  suala hili linatakiwa liangaliwe kwa kina na lipatiwe ufumbuzi ili kuendana na mfumo wa dunia kwani nchi tunazoona zimeendelea pia zimewekeza vya kutosha kwenye duru ya michezo.

Suala jingine ni mipango mibovu pamoja na maandalizi yasiyo rizisha. Mathalani iwe ni masumbwi, mpira wa magongo, riadha n. k yaani timu na wachezaji hawaandaliwi vya kutosha ikiwa ni pamoja na muda mfinyu wa maandalizi, pia kumekuwa hakuna mipango endelevu ya kuweza kuimarisha sekta hii kwa mfano mashindano yakitokea ndipo husikia wachezaji wameitwa kambini maandalizi siku chache tu Kisha wanaenda kwenye mashindano wakiwa hawana maandalizi ya kutosha kimwili kiakili kisaikolojia wa kiufundi kinachofuata ni kutolewa mapema na kutoa fursa kwa vyombo vya habari kutumia msemo pendwa wa "TANZANIA NI KICHWA CHA MWENDAWAZIMU" inawezekana ikawa kweli lakini huu uendawazimu tunajitakia tu.

Tazama wenzetu wanaofanya vizuri utakuta mipango yao ni ya muda mrefu na endelevu timu na wachezaji wnaandaliwa kwa muda mrefu kabla ya kwenda kwenye mashindano na hatimaye kufanya vizuri. Mh Nape tunaomba nasi tuwe na mpango endelevu yenye tija ili angalau kwa miaka mitano uliyoaminiwa na Rais umuoneshe kuwa unaweza na hakukosea kukuweka wewe hapo ulipo.

Kuna suala la vifaa vya kimichezo nalo Tanzania bado tumekuwa tukicheza Pata potea. Yaani kumekuwa na uhaba pamoja na ukosefu wa vifaa vya kimichezo na hata vikiwepo basi navyo utakuta ni Duni yaani haviwezi kutosheleza mfumo wa kisasa wa kimichezo. Hapa panahitaji uwekezaji wa kutosha ili tuweze kuboresha huku ili Tanzania iwe na heshima walau hata kwa michezo kadhaa. Hivyo Mh ni jukumu lako kuhakikisha uwekezaji wa nguvu unaelekezwa katika michezo walau hata kwa kiasi kidogo kitakachopatikana kiweze pia kutumika vizuri.

Rasilimali watu pia lazima itazamwe katika michezo. Hapa namaanisha kwamba wanamichezo kwa ujumla ni lazima waandaliwe na wathaminiwe. Ni jambo la wazi kabisa kwa nchi yetu ya Tanzania lipo na ni kawaida tu kukuta mchezaji hathamini hata kidogo lakini huyo huyo ndiye baadaye anatakiwa akaliwakikishe Taifa sasa kinachotokea ni kuwa yeye hafanyi kazi kwa kujitoa kwa sababu waliomtuma hawamthamini hata kidogo.

 Ni jambo la kisikitisha kuona wachezaji wengi wakiwa hawathaminiwi Kulingana na michezo yao matokeo yake tukienda kwenye mashindano tunakuwa washiriki tu na sio washindani huku tukitolewa mapema na kuahidi tutajipanga kwa ajili ya mwakani mwakani ukifika inakuwa yale yale.

Waswahili wana msemo wao kuwa "Samaki mkunje angali mbichi" haimaanishi kuwa akikauka hawezi kukunjika Hapana, anaweza kukunjika,lakini atavunjika. Vivyo hivyo katika michezo mchezaji au mwanaspoti yoyote yule ni sharti aandiliwe tangu akiwa bado mdogo ili akikuwa awe na uelewa wa kutosha wa mchezo huo, uzoefu pamoja na uhodari katika mchezo husika. Tanzania Kisiwa cha amani imekuwa ni tofauti sana yaani hatuna kabisa Utamaduni huu.

 Matokeo yake ni timu zetu za Taifa na zile za vilabu kuboronga katika ngazi ya Kimataifa. Mfano mzuri ni wenzetu wa Nigeria wameamua kuwekeza kwa vijana /watoto na matunda tunayaona hii LEO.UMISETA /UMITASHUMTA /COPA COCACOLA hivi vipo japo viliondolewa na kureheshwa hivi karibuni. Mimi binafsi naamini kuwa licha ya kuwa vina msaada katika sekta ya Michezo kwa kuibua vipaji Lakin ni wazi kuwa havina msaada katika suala la kukuza na kuendelea vipaji. Kinachotakiwa ni kuwa zijengwe shule maalum kwa ajili ya kuwafundisha kuwajenga na kuwalea watoto Hawa waliopatikana kutoka UMITASHUMTA UMISETA COPA COCACOLA waweze kulelewa na kutuzwa hapo.

 Watakuwa katika misingi ya kimichezo. Na izi shule ziwe kama shule nyingine na michezo ndiyo iwe masomo yao na wala wasiwaze mambo mengine zaidi ya Michezo tu, hapo tutakuwa tunatengeneza kizazi cha vijana ambao watakuwa na Msaada hapo mbeleni Kati sekta ya Michezo Na kuikwamua Tanzania kutoka hapa ilipo hadi hatua ya juu zaidi. Pia tuwe na Utamaduni wa kuwapeleka watoto wanaonekana kufanya vizuri za katika Academy za wenzetu Ulaya ili wakafundishwe huko na ikiwezekana wacheze huko huko katika vilabu mbalimbali kama vile soka na mpira wa kikapu. Kufanya hivyo watajua aina ya Michezo linalochezwa Ulaya na mabara mengine.

Tusiishie tu kwa wachezaji bali lazima tuwafundishe walimu wa kutosha ambao itakuwa ni hazina ya kwetu badala ya kuwa tunaagiza makocha kutoka nje na kuwalipa gharama kubwa bila ya mafanikio yoyote. Badala ya kununua makocha kutoka nje badala yake tuajili wakufunzi wachache watakaofundisha walimu wazawa ikiwa ni pamoja na waamuzi ili kuwa na hazina ya watu ya kutosha kuweza kuinua sekta hii pendwa na kurejesha
Heshima ya nchi yetu kimichezo.

Hayo pamoja na mengine mengi yakizingatiwa basi sekta ya michezo itafanya vizuri na kuieletea nchi yetu heshima Kimataifa.

Imeandaliwa na Shaaban Maulidi
0718526159/0763902318.
USHAURI WANGU KWA NAPE, WAZIRI WA HABARI, MICHEZO NA UTAMADUNI. USHAURI WANGU KWA NAPE, WAZIRI WA HABARI, MICHEZO NA UTAMADUNI. Reviewed by WANGOFIRA on 21:34:00 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.