NAIBU WAZIRI WA MIUNDOMBINU NA USAFIRISHAJI UDSM APIGWA RISASI, AFARIKI PAPO HAPO.



Naibu waziri wa miundombinu na usafirishaji chuo kikuu cha Dar es salaam ambaye pia ni mwanafunzi wa mwaka wa nne katika chuo kikuu hicho Bw. Mutaengerwa Mafwiri, amefariki dunia baada ya kupigwa risasi na watu wanaosadikika kuwa ni majambazi, katika eneo la Ubungo Msewe.

Mashuhuda wa tukio hili wanaeleza kuwa marehemu amefikwa na mauti hayo mara baada ya kutoka nje kwa ajili ya kwenda kushangaa kitu kilichozaniwa kuwa ni mlipuko wa transfoma ndipo alipofyatuliwa risasi na majambazi ambao walikuwa wanapora na kuvamia maduka yaliyo maeneo ya Ubungo Msewe.

Wangofira Blog inaendelea kufuatia undani wa tukio hili kwa vyombo vya ulinzi na usalam ili kujua ni hatua zipi zinafuata ili kuaga mwili wa marehemu na kuusafirisha kwao kwa mazishi.
Ikumbukwe kuwa hii si mara ya kwanza kwa wanafunzi wa chuo kikuu cha dar es salaam kuuwawa kwa kupigwa risasi na matukio mengine kama wanafunzi kufa kwa kugongwa na magari pale wanaporudi maeneo walipopanga, kwani mwaka jana wanafunzi wawili wa chuo kikuu hiki pia waliuwawa kwa kupigwa risasi na wengine kujeruhiwa wiki mbili zilizopita maeneo ya mabibo hosteli.
MUNGU AILAZE PEMA ROHO YA MAREHEMU MAHALI PEMA, AMENI.


-
NAIBU WAZIRI WA MIUNDOMBINU NA USAFIRISHAJI UDSM APIGWA RISASI, AFARIKI PAPO HAPO. NAIBU WAZIRI WA MIUNDOMBINU NA USAFIRISHAJI UDSM APIGWA RISASI, AFARIKI PAPO HAPO. Reviewed by WANGOFIRA on 13:28:00 Rating: 5

1 comment:

Powered by Blogger.