HONGERA JOB NDUGAI KUWA SPIKA WA BUNGE LA 11.

Mbunge wa Kongwa (CCM) Job Ndugai ameshinda kiti cha Uspika kwa kura 264 sawa na kura asilimia 70 huku mpinzani wake Goodluck Ole Medeye kwa tiketi ya chadema akipata kura 109 sawa na asilimia 30, huku wagombea wengine wakipata kura 0.

Job Ndugai alikuwa naibu spika wa bunge la 10 chini ya spika Anne Makinda, kwa kuongoza kwa kipindi cha miaka 10 katika nafasi hiyo na kwa sasa anakuwa Spika wa Bunge la 11 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. 

Mungu ibariki Tanzania, Mungu libariki bunge la 11 ili liwatumikie watanzania ipasavyo.
HONGERA JOB NDUGAI KUWA SPIKA WA BUNGE LA 11. HONGERA JOB NDUGAI KUWA SPIKA WA BUNGE LA 11. Reviewed by WANGOFIRA on 03:00:00 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.