Utalii

MILIMA YA UDZUNGWA
Mwandishi; Baraka Ngofira
Baada ya kuwa tumeangalia vizuri utalii unaofanyika katika visiwa vya Zanzibar ambapo ulifurahi japo kwa kusoma na kuhadithiwa tu msomaji wangu , leo tutaangalia kivutio kingine kinachopatikana nchini Tanzania japo vipo vingi ambavyo nitakuwa ninakudadavulia kila wiki katika kona hii ya Utalii. Nikukumbushe tu japo kwa ufupi kuwa Zanzibar ni kisiwa ambacho kina vivutio vingi vya kitalii ambapo tuliona kama vile vya mji mkongwe, nyangumi wanao ruka hewani na kutumbukia majini, misitu, kima wekundu na vivutio kibao vinavyopatikana huko.
Leo tutasangalia kivutio kingine cha kitalii kinachopatikana kwenye mji maarufu hapa nchini si mwingine ni mji kasoro bahari au mkoa wa Morogoro. Mkoa wa morogoro ni mkoa maarufu sana hapa nchini ambapo watu wengi hupenda kuishi na wengine wafikapo Morogoro basi uona kama kiu yao ya maendeleo imefika pahali pake.
Ni mkoa maarufu kwa ulimaji wa miwa katika bonde la mto Kilombero ambapo miwa mingi hulimwa na kuzalisha sukari nyingi ambayo hutumiwa nchini na nyingine huuzwa nje. Pia ni mkoa maarufu kwa uzalishaji wa mchele na mahindi na mazao mengine kama vile vitunguu na mengine mengi.
Vivutio vya kitalii vipatikanavyo mkoani humu ni mbuga ya Selous,hifadhi ya taifa ya mikumi, milima ya udzungwa, mto kilombero na vingine vingi lakini leo tuangalie kwa undani mlima ya udzungwa ambayo inapatikana mkoani morogoro na sehemu kidogo katika mkoa wa Iringa. Kabla ya kuja kwa wakoloni milima hii ilijulikana kama wadsungwa jina ambalo wenyeji wa kipindi hicho waliita milima hiyo kabla ya ujio wa wakoloni wa kijerumani waliiobadili jina na kuuita Udzungwa.
Milima hii ni hifadhi yenye ukubwa wa takribani kilomita za mraba 1990, iko umbali wa kilomita 350 kusini mwa Dar es salaam, na kilomita 65 kutoka hifadhi ya Mikumi. Kama ilivyokuwa kwa Zanzibar milima hii nayo ina vivutio ambavyo ni hadhimu sana kupatikana katika sayari bali vinapatikana katika milima hii pekee, Wakiwemo wanyama, misitu, ndege, na vitu vingi vya kuvutia.
Wapo Mbega wekundu wa Iringa  “ Iringa red colobus Monkey” na wale Sanje “Sanje Crested Mangabey” ambaye alijulikana mwaka 1970 ambao hawapatikani mahali pengine tofauti na milima hii, na hivyo kuwa kivutio kikubwa kwa watu kutoka nje ya nchi kuja kuwatazama na kulipa pesa nyingi. Lakini bado watanzania hatuna aya kuona wageni wanakuja kutazama wanyama wetu si tumelidhika kabisa na wala hata hatushituki tunabaki kuwashangaa wageni, kwa kuwa wao wanakuja kutazama wanyama ambao sisi tunao kila siku.
Piandani ya milima hii kuna maeneo ya kiutamaduni na kihistoria ambapo shughuli mbalimbali za kijadi , kitamaduni hufanyika ikiwemo ibada za kimila ambapo wenyeji hufanya maagano na matambiko kwa miungu wao. Kwa kweli inapendeza ukiona kwa macho yako jinsi mahali hapa palivyo pazuri na pakuvutia. Bokela au mlima wa mungu ni moja ya eneo la ibada pia yapo maeneo ya pango la Mwanaruvele na pango la nyumbanitu, na milima ya Ndundulu. Ni maeneo makubwa ya kihistoria yanayovutia watu kutoka kona zote za dunia kuja kutazama maajabu ya milima hii maarufu ya Udzungwa.
Ukiachilia mbali maeneo ya kihistoria na kitamaduni kuna ndege ambao wanapatikana katika milima hii pekee, si wengine bali ni Chozi bawa jekundu au kwa kimombo “ Rofous winged sunbird” na jamii mpya yak wale iliyogundulika mwanzoni mwa mwaka ya 1991. Ambao hujulikana kama kwale misitu jamii hii ya ndege ni ya ajabu kutokana na rangi yake kuvutia na kungaa san na hivyo kufanya watalii kufurahia maajabu ya ndege hawa. Pia jinsi ndege hawa wanavyoishi ni tofauti na ndege wengine hivyo waweza jua jinsi walivyo ndege wa maajabu kwa kweli.
Pia kuna miti ya ajabu ambayo hukiwa muoga unaweza kudhani kuwa ni nyoka mkubwa anapanda juu ya mti bali ni miti ambayo imejivilingisha vilingisha mfano wa nyoka. Haya nayo ni maajabu ya Mungu nay a kuvutia yanayopatikana katika milima hii ya Udzundwa.
Maporomoko ya maji yenye urefu wa kilomita 170 yakianguka kupitia misitu ya kututa mithili ya mianzo ya ukungu bondeni, nayo ni kivutio tosha cha kuwawezesha watalii kuja kutazama na kutembelea milima hii ya udzungwa, kwao ni faraja kuonda kwa macho yao lakini kwa watanzania walio wengi wao upenda kuhadhithiwa tu maajabu na uzuri wa maajabu haya ya Mungu ambayo watanzania tumepewa na nchi nyingine watatamani wangekuwa wayo. Au, ndiyo kusema kuwa mwenye nacho hakithamini? au penye miti hapana wajenzi? au nabii hakubaliwi kwao?. Jiulize mtanzania mwenzangu kwa nini hautembelei wala kuona uthamani wa vivutio vyetu tulivyonavyo? Kazi kwako Mtanzania.
Pia kuna ua ambalo limebatizwa jina la African Violet au ua la kiafrika ambalo linapatikana ndani ya hifadhi hii, katikati ya miti mirefu yenye mita takribani 30 hivi. Ambazo huwa kivutio kikubwa kwa watalii wote wa ndani na wale wa nje ambao hupata fursa za kutembelea hifadhi hii kujionea uumbaji na maajabu ya Mungu katika milima hii ya Udzungwa.
barakangofira@gmail.com
Utalii Utalii Reviewed by WANGOFIRA on 02:58:00 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.