MLIMA MERU

MLIMA MERU, UNAVYOIPENDEZESHA ARUSHA

Image result for jiji la arushaImage result for jiji la arushaImage result for mlima meru



Na,
Baraka Ngofira
Tanzania ina majiji matano ambayo ni Arusha, Mbeya, Tanga, Mwanza na Dar es salaam. Kila jiji linavioja vyake na vivutio vyake mfano mwanza watu wengi hupaita mji wa miamba maarufu kama The Rock  City ufikapo jijini hapa madhari nzuri na ya kupendeza ikisaidiwa na upepo mwanana wa ziwa Victoria. Milima na mawe mazuri yapatikanayo maeneo ya Kopripoint ambayo yanaupendezesha mji huu wa miamba kuwa kivutio kikubwa cha kitalii.
Ukitoka Mwanza ukija Tanga upepo mzuri kutoka bahari ya Hindi, mapango ya Amboni na fukwe nzuri pasipo kusahau mbuga nzuri ya wanyama ya Saadani yenye wanyama wazuri na wa kuvutia.
Pia jiji la Mbeya likisika kwa kijani chake kutokana na kuwa na hali ya ubaridi baridihivyo kupelekea watu wengi kulima mazao mbalimbali ya chakula ikiwemo mahindi na mpunga pasipo kusahau matunda. Pia jijini hapa kuna vivutio vingi sana vya kitalii ikiwemo maporomoko ya maji na mabonde mengi makubwa yanayofanya  jiografia ipendeze na kuvutia.
Ukiachilia mbali majiji haya lipo jiji maarufu Tanzania wengi wakiliita eti mjini au Town na msanii mmoja wa bongo fleva akaimba usije mjini. Ni jiji  la kibiashara lililojaa pilikapilika za hapa na pale na kuwa na vivutio vingi pamoja na maeneo mengi ya kihistoria ikiwemo makumbusho ya taifa, na nyumba ya makumbusho iliyopo Kijitinyama.
Leo tuangalie jiji la kitalii wengi wakiliita A town lakini kwa wazawa wakiliita R chuuuga hii ni kutokana na sifa mbalimbali wanazozifahamu wenyeji wa jiji hili.
Jiji la Arusha limekuwa jiji maarufu kwa utalii hasa kutokana na kuwepo vivutio vingi vya kitalii pia hali ya hewa ya ubaridi inayovutia watalii wengi hususani wanaotoka nchi za ulaya na asia ambapo kuna hali ya hewa ya ubaridi.
Leo tuangalie moja ya kivutio maarufu saana jijini Arusha japo wengi hawaoni kama kuna umuhimu wake na kutothamini mchango wake kwa maendeleo ya sekta ya utalii hapa nchini. Si kivutio kingine bali ni mlima Meru upatikanao jijini Arusha ikiwa ni takriban kilomita 35 kutoka uwanja wa kimataifa wa Kilimanjaro maarufu kama KIA.
Mlima Meru ni mlima wenye tabia ambazo ni tofauti na milima mingine ipatikanayo hapa nchini ikiwemo Kilimanjaro, udzungwa japo kidogo unakaribiana sifa na mlima maarufu na mrefu wa Kilimanjaro. Ni mlima wa 72 kwa urefu duniani, wa 5 barani  Afrika na wa 2 nchini Tanzania ukiwa na urefu wa mita 4565 kutoka usawa wa bahari ambao ni sawa na futi 15064.
Unapatikana ndani ya hifadhi ya Arusha iliyoanzishwa mnamo mwaka 1960 ambayo ina ukubwa wa kilomita za mraba 137 huku ikiwa na wanyama kama vile tembo, nyati, nyani na wengine wengi amabao ujipatia maisha na riziki zao ndani ya mlima huu.
Huku ukiwa na sifa kama za mlima Kilimanjaro, mlima Meru naon imlima wa volcano hai ambayo inasadikika iliwahi kuripuka miaka milioni 6 iliyopita. Hivyo basi kuufanya mlima huu kuwa na upekee na wa kuvutia uwapo Arusha unaonekana vizuri kuanzia mwezi june hadi wa februari na kufanya watalii wengi kuja kutembelea miezi hiyo.
Wataalam wa mlima huu udai kuwa kupanda mlima huu ni zoezi gumu sana ikilinganishwa na mlima Kilimanjaro kwani uchukua siku tatu hadi nne, kukamilisha kupanda na kushuka kwenye mlima huu. Na endapo mtalii au yeyote anayepanda mlima huu akiwa kasi sana hushauriwa apunguze kasi kwani ni hatari sana kwa usalama wa afya yake.
Una vilele viwili kama ilivyo kwa kibo na mawenzi kwa mlima Kilimanjaro, kwa mlima Meru kuna kilele cha Meru kubwa ambacho kina urefu wa mita 4565 na ndiyo kilele ambacho uonekana na watu wengi hasa wafikapo Arusha. Na kilele kingine ni Meru ndogo ikiwa na urefu wa mita 3820 ambacho uonekana ukiwa ndani ya hifadhi ya Arusha. Na hivyo kuwa na sifa za kipekee ambapo muda mwingi huwa kilele hiki kimefunikwa na mawingu na barafu.
Pia mlima huu umezungukwa na misitu ambayo imekuwa rafiki sana wa wanyama pori wakiwemo fisi, nyani, mbega wekundu  pundamilia, tembo, nyoka , mbwa mwitu, simba na chui japo muda mwingi huwa hadhimu sana kuonekana kwa muda wote kutokana na wanyama hawa hifadhini hapa hii ni kutokana na wao kuwa na sifa tofauti na wanyamapori wengine wa mbuga kama ya Serengeti na Ngorongoro.
Ndani ya misitu huu pia wamo ndege aina ya flamingo na Heroe ambao wamekuwa kivutio kikubwa cha kitalii kutokana na jamii hii ya ndege kutopatikana kwenye hifadhi nyingi za hapa nchini.  Na sifa yao kubwa ya kutaga mayai katika ziwa Natron na baada ya kuaguliwa vifaranga urudi kujipumzisha katika ziwa Momella ambapo kuna mazingira ya tulivu. Hivyo kuipa sifa za kipekee misitu hii ya mlima Meru.
Pia uwepo wa ziwa Momella na Rishani ambayo yamekuwa rafiki wa karibu kwa wanyama pori hawa kutokana na kuwa na maji ya alkaline au chumvi chumvi ambayo usaidia wanyama hawa kuishi pasipo shaka na shida yoyore wawapo ndani ya hifadhi hii.
Lakini uajabu wa maziwa haya ni kutokuwa na mito yoyote ya kuingiza wala kutoa maji lakini kamwe maziwa haya hayakauki mwaka mzima. Bila kujali ni kiangazi au ni wakati wa masiak na hivyo kufanya viboko kuishi kwa raha mstarehe kabisa.
Pia uwepo wa crater ya Ngurudoto imekuwa kivutio kikubwa sana cha kitalii hifadhini hapa ikiwa na ina ukubwa wa kilomita 10.63 na kina chake kikiwa na urefupi wa mita333.


                  Image result for mlima meru
 Watalii utumia muda wao mwingi kushangaa na kupiga p[icha kama sehemu ya kuweka kumbukumbu. Crater hii ina sehemu kadhaa za nje ambapo mara nyingi usimama eneo la Rhino Point ambapo watu usimama na kutazama vizuri jinsi Mungu alivyoweka maajabu haya ikiwa ni pamoja na wanyama wanaopatikana hifadhini hapa
Maporomoko ya maji ya ya Tululusia na Maio yenye urefu wa mita 28 na yakiwa karibu kabisa na njia ya kaskazini ya kupandia mlima Meru ambapo mtalii afikapo hapa lazima ashuke ili haweke ukumbusho kwa picha mgando au zile za mwendo maarufu kama video.
Tao la mti wa mkuyu au kwa kingereza linaitwa Fig tree Arch, kivutio hichi ni cha ajabu kwani gari lenye ukubwa wa tembo uweza pita katikati  pasipo na shida yeyote linalo ongoza watalii kupanda mlima meru lazima lipite hapa. 

              Image result for mlima meru

Ni mti wenye historia ndefu na maajabu ambapo majani yake kamwe hayawezi kudondoka.
Hivyo basi wewe kama mtanzania ni lazima uweze kutembelea hifadhi hii na  mlima Meru ili uweze kujionea mengi ya maajabu na vivutio mbalimbali vya kitalii vilivyopo hapa nchini. 
MLIMA MERU MLIMA MERU Reviewed by WANGOFIRA on 00:49:00 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.