EPAINETO PUMZIKA KWA AMANI UKINGOJEA PARAPANDA.http://wangofira.blogspot.com/2015/10/epaineto-pumzika-kwa-amani-ukingojea.htmlhttp://wangofira.blogspot.com/2015/10/epaineto-pumzika-kwa-amani-ukingojea.htmlA



Utakumbukwa daima, kaka yetu tuliyekupenda sana, ndugu Epaineto Mujaya. Sauti yako haitasahaulika hasa watu watakapotazama nyimbo zako hususani ulipokuwa kwaya ya kamnyonge " eeeeh Mungu wa vyote"

Pia, idara ya vijana itakukumbuka ndugu yetu, Epaineto Mujaya, sijui ni lugha gani nielezeee lakini tuliobaki tutakukumbuka kwa yote mema uliotufanyia kipindi cha uhai wako.

Lakini pia sijui kwa mini umeondoka kipindi hiki ambacho kwaya ya kamnyonge ikiwa na hitaji kubwa na wewe ndugu yetu Epaineto Mujaya. Sina lugha nyepesi ya kusema nikiwa nazisikiliza na kutazama nyimbo zako ulizopewa uwezo wa kuzitunga enzi za uhai wako.

"Eeeh Mungu wa vyote Mungu wa rehema nimejifunza kukutumainia" ni moja ya wimbo uliobeba tafakari kuu, ambao wengi watakuikumbuka sauti na busara zako katika utunzi huu wa nyimbo za injili.

Swali la kujiuliza yeye ametangulia mbele ya haki, siku yetu itafikaje na je utakufa kifo gani. Na historia gani utakayoiacha hapa duniani. Yeye tutamkumbuka kwa utunzi wake Mwema ambao umetukuka katika historia ya mziki wa injili. Buriani kaka Epaineto Mujaya daima tutakukumbuka daima.
Kifo chako kumetugusa sisi kama wanakamnyonge na wengine tuliokufahamu vyema.

Upumzike kwa amani huku ukingoja ufufuo tukaurithi uzima wa milele.http://mtangazaji.blogspot.co.ke/2015/10/wadau-wa-muziki-wa-injili-katika-kanisa.html
EPAINETO PUMZIKA KWA AMANI UKINGOJEA PARAPANDA.http://wangofira.blogspot.com/2015/10/epaineto-pumzika-kwa-amani-ukingojea.htmlhttp://wangofira.blogspot.com/2015/10/epaineto-pumzika-kwa-amani-ukingojea.htmlA EPAINETO PUMZIKA KWA AMANI UKINGOJEA PARAPANDA.http://wangofira.blogspot.com/2015/10/epaineto-pumzika-kwa-amani-ukingojea.htmlhttp://wangofira.blogspot.com/2015/10/epaineto-pumzika-kwa-amani-ukingojea.htmlA Reviewed by WANGOFIRA on 11:40:00 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.