TANGAZO LA KAZI WIZARA YA KILIMO NA UVUVI




JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA KILIMO CHAKULA NA USHIRIKA



                                                                            

TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI

Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika anawatangazia Watanzania wote wenye sifa zilizoanishwa hapa chini watume barua za maombi ya kazi zifuatazo.

1.         Afisa Utafiti Kilimo Daraja la II (Agricultural Research Officer II) Nafasi 70

            (aSifa za waombaji                                                                                                    

          Wawe wamehitimu Shahada ya Kilimo (Bsc Agriculture General), Uchumi Kilimo, Uhandisi Kilimo, Food Science and Technology, Biotechnology Laboratory Sciences, Agronomy,Bsc Environmental Science  na Horticulture kutoka chuo kinachotambuliwa na Serikali.  
      

(b)  Majukumu

Ø  Kusaidia kukusanya na kuandika ripoti za utafiti chini ya maelekezo ya Afisa Utafiti Kilimo Mwandamizi.

Ø  Kukusanya, kurekodi na kuchanganua takwimu za kazi za Utafiti zinazoendelea.

Ø  Kusaidia katika kuendesha semina na kuwaelekeza wakulima jinsi ya kutumia teknolojia mpya  kwa kuzingatia hali ya uchumi na mazingira yake.

Ø  Kutoa ripoti ya maendeleo ya Utafiti na mapendekezo ya Utafiti katika Mikutano ya kanda.

Ø  Kufanya shughuli za Utafiti chini ya maelekezo na uangalizi wa Afisa Utafiti Kilimo Mwandamizi.
Ø  Pamoja na kazi nyingine za Utafiti kama atakavyopangiwa na kiongozi wake wa kazi.

(c)       Mshahara

Ø  Mishahara ya Watumishi wa Serikali ngazi ya TGRS A.  



2.            Mhandisi Kilimo Daraja la II (Agro Engineer II). Nafasi 88

            Waombaji watakaochaguliwa watapangiwa kazi Wizara ya Kilimo chakula na Ushirika    na Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI).


(a)          Sifa za waombaji

Ø  Wawe wamehitimu Shahada ya Uhandisi yenye mwelekeo mkubwa katika fani ya Kilimo, Umwagiliaji,Ujenzi,Ufundi na Mazingira  kutoka Chuo Kikuu kinachotambuliwa na Serikali

(b)          Majukumu

Ø  Kuandaa program za mafunzo kwa wakulima kutumia zana za Kilimo

Ø  Kushirika katika kufundisha wakulima na matumizi bora ya zana.

Ø  Kushiriki katika ujenzi wa miradi ya Umwagiliaji

Ø  Kushiriki kutengeneza michoro/ramani za umwagiliaji.

Ø  Kukusanya takwimu za miradi ya umwagiliaji

Ø  Kufuatilia program za mafunzo ya wanyamakazi mafundi wa matrekta wa wakulima jinsi ya matumizi ya wanyama kazi na matrekta

Ø  Kushiriki kuratibu na kutoa huduma za umwagiliaji pamoja na matumizi ya maji.

Ø  Pamoja na kazi zingine atakazopangiwa na mkuu wake wa kazi.

Ø  Kupitia mapendekezo ya miradi mbalimbali ya ufundi yanayowasilishwa Wizarani.

Ø  Kusimamia mikataba ya ujenzi/ukarabati wa miundombinu ya umwagiliaji.

Ø  Kushirikiana na mafundi sanifu kuwafundisha wakulima uendeshaji wa skimu za umwagiliaji

(c)          Mshahara

Ø   Mishahara ya Watumishi wa Serikali ngazi ya TGS E.

3.            Afisa Kilimo Daraja la II (Agro – Officers II) Nafasi 378
Waombaji watakaochaguliwa watapangiwa kazi Wizara ya Kilimo chakula na Ushirika na Wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI).


(a)          Sifa za waombaji

Ø  Wawe wamehitimu Shahada ya Sayansi Kilimo (Bsc.Agriculture General,Bsc.Horticulture,Bsc.Agronomy,Bsc.Environmental Sciences) na Mazingira kutoka Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine au vyuo vingine vinavyotambuliwa na Serikali.

(b)          Majukumu

Ø  Kudhibiti visumbufu vya mazao na mimea

Ø  Kukusanya takwimu za bei za mazao kila wiki na kila mwezi

Ø  Kukusanya takwimu za upatikanaji wa mazao katika masoko kila wiki/mwezi

Ø  Kuendesha mafunzo ya wataalamu wa Kilimo

Ø  Kufanya ukaguzi wa ubora na matumizi ya pembejeo na zana.

Ø  Ufuatiliaji wa mwenendo wa soko la mazao ya biashara

Ø  Kuendesha mafunzo juu ya hifadhi bora ya udongo na maji

Ø  Kutoa habari juu ya teknolojia mpya kwa wadau

Ø  Kuandaa/ kuandika taarifa za utekelezaji kwa sekta ndogo ya mazao.

Ø  Kusimamia/kuendeleza taaluma ya uzalishaji mboga, matunda, maua na mazao mengine.

Ø  Kusimamia/kuendeleza uzalishaji wa mbegu bora

Ø  Kuandaa, kutayarisha, kufunga na kusambaza mbegu bora

Ø  Kufanya ukaguzi wa mbegu mpya kwa kushirikiana na Watafiti wa mbegu kabla kupitishwa

Ø  Kuendesha mafunzo ya kuzalisha mbegu matunda, maua na viungo

Ø  Kuhamasisha uzalishaji wa mazao ya bustani

Ø  Kufanya utafiti mdogo mdogo wa mazao yanayofaa kulimwa katika sehemu ya Kilimo cha Umwagiliaji.

Ø  Kufanya utafiti wa udongo

Ø  Kuhamasisha uanzishaji wa vikundi vya wakulima/ wamwagiliaji
Ø  Kuzalisha mbegu za msingi baada ya kuzalishwa na watafiti

Ø  Kuendesha/kusimamia vishamba vya majaribio vya mbegu na uchunguzi maabara ili kuondoa utata juu ya mbegu.

(c)          Mshahara

 Mishahara ya Watumishi wa Serikali ngazi ya TGS D.

4.            Mkufunzi Kilimo Daraja la II (Agricultural Tutor II) Nafasi 38
  Waombaji watakaochaguliwa watapangiwa kazi ya kufundisha katika vyuo vilivyo chini ya Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika na Wizara ya  Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi.


            (a)       Sifa za waombaji

Wawe wamehitimu Shahada ya kwanza yenye mwelekeo wa Kilimo (Bsc.Agriculture        General,Bsc.Agricultural Engineer,Bsc. Agronomy, Bsc.Irrigation Engineer)  kutoka Chuo Kikuu cha Kilimo- Sokoine au Chuo kingine kinachotambuliwa na Serikali.

            (b)       Majukumu
                    Kufundisha kozi za stashahada na astashahada za kilimo  nadharia na vitendo

Ø  Kuandaa mtiririko na mpangilio wa masomo (Lesson Sequences and Plans)

Ø  Kusoma na kuelewa vema mihutasari ya mafunzo na kuitafsiri kwenye masomo

Ø  Kuandaa na kufundisha kozi za wakulima

Ø  Kuandaa na kupanga somo la vitendo na kusimamia wanachuo wakati wa kujifunza

Ø  Kupima maendeleo ya wanachuo kwenye mitihani kwa kipindi chote kinachohusika na kutunza alama zao.

Ø  Kupima maendeleo ya wanachuo kwa kushirikiana na Maafisa Kilimo wa Wilaya/Viwandani wakati wa mafunzo kwa vitendo (Field Practicals).

Ø  Kutekeleza shughuli nyingine za kikazi kadri atakavyopangiwa na Mkuu wake wa kazi.

            (c)       Mshahara

Ø  Mishahara ya Watumishi wa Serikali ngazi ya TGS D.

Waombaji wote katika barua zao ni lazima waonyeshe sehemu ambayo wangependa kupangiwa kwa nafasi zile zinazohusisha zaidi ya wizara moja. Hata hivyo uamuzi wa mwisho juu ya vituo ni wa mwajiri/ Mamlaka za ajira ambako nafasi zinapatikana.
\




MAMBO YA KUZINGATIA
Barua za maombi ziambatane na Curriculum Vitae (CV), picha ndogo mbili ukubwa wa pasipoti, cheti cha kuzaliwa, vivuli vya vyeti vya kuhitimu elimu ya sekondari na Shahada husika .

Waombaji wawe na umri usiozidi miaka 45.

Wahitimu walioajiriwa Serikalini hawaruhusiwi kuomba nafasi hizi kwasababu tayari wana ajira
Wahitimu waliotuma maombi yao kabla ya tangazo hili wanashauriwa kutuma maombi upya.

Barua zote za maombi ziwasilishwe katika  muda wa siku 14 kuanzia
tarehe ya kwanza ya kuonekana tangazo hili.

Tangazo hili linapatikana pia kwenye tovuti ya Wizara, www.kilimo.go.tz



Barua za Maombi zitumwe kwa:

            Katibu Mkuu,
            Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika,
            S.L.P. 9192,

            DAR ES SALAAM.
TANGAZO LA KAZI WIZARA YA KILIMO NA UVUVI TANGAZO LA KAZI WIZARA YA KILIMO NA UVUVI Reviewed by WANGOFIRA on 07:45:00 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.