Je unajengaje heshima yako binafsi?


Kujiheshimu ni maana ya vitu vya msingi ndani ya maisha ya mtu mwenyewe. Tukikosa kujiheshimu tunaanza kupambana ndani ya nafsi zetu huku tukijitahidi kuwa kama mtu fulani.
11709513_445949675584943_3616026047559487528_n
Mtangazaji wa TV wa Kenya, Sarah Hassan
Kitu ambacho unatakiwa kujua kujiheshimu ni kuwa na ujasiri wa kutunza na kuendeleza ujasiri uliopo ndani yako haijalishi umekutana na jambo gani kwenye maisha ya kila siku. Hapa tunakupa baadhi ya mambo kadhaa ya kukusaidia kujenga heshima yako;
1. Simamia maisha yako mwenyewe
Tuna msukumo mkubwa kutoka kwa wazazi, kazini na jamii inayokuzunguka wakikutaka uwe wa namna fulani hivi. Huo msukumo ni vigumu sana kuukimbia, lakini heshima kubwa inatokana na kile ulichonacho ndani yako.
Ni muhimu wewe mwenyewe uwe na misingi ya tabia na mwenendo ambao utausimamia na kuishi nao. Hii haimaanisi kwamba kila mtu akikwambia unatakiwa uwe hivi au vile wako sawasawa, hapana kila mtu anatakiwa kuchagua njia ya kwenda na kuona umuhimu wake. Hebu fikiria kama ulizaliwa ili uweze kumfurahisha jirani yako au rafiki yako? Unatakiwa kuishi maisha yako wewe kama wewe si kuiga kwa mtu mwingine.
2. Jifunze kukabiliana na upinzani
Sisi kama binadamu tuna hulka ya kukasirika au kughafirika tunapokutana na upinzani, wengi hatupendi kupingwa wala hatutaki kuonekana tunapingwa . Ili kujenga heshima yako inakubidi ujifunze namna ya kukabiliana na upinzani, uangalie mama kwa mapama yake sana na usiyachukulie kibinafsi zaidi. Kama upinzani unaoupata si wa kweli, achana nao na kama ni wa kweli unaweza kuutumia kujijenga na kujifunza tabia njema.
3. Angalia mwonekano wako kwa ukaribu bila kuwa mtumwa wa mitindo
Mwonekano wetu ni muhimu, inatupa ujasiri. Hivyo simamia kwa umakini jinsi unavyovaa lakini kwa wakati huo huo usije ukageuka mtumwa wa mtindo ya mavazi. Vaa kwa manufaa yako binafsi na si kwa kujaribu kuwafurahisha watu fulani.
4. Ondokana na wivu
Wivu kwa watu wengine kuona jinsi walimvyofanikiwa ni njia ya kawaida sana inayosababisha mtu kukosa amani na furaha na vile vile unajikuta hujiheshimu tena. Unapoendelea kujilinganisha na mtu mwingine ni rahisi sana kupoteza malengo yako ya maisha, utajikuta unafanya kwa sababu ya kujishindanisha. Hii haimaanishi kwamba usiangalie watu wengine wanafanya nini bali baada ya kuangalie wenzako wamefanikiwaje unaamua kufanya nini? Usipoteze malengo yako kwa kufanya vitu ambavyo havihusiani na wewe utajikuta ukipoteza mwelekeo kabisa.
5. Kumbuka hamasa yako na wala si matokeo yako
Wakati mwingine tunafanya sana kazi kulingana na hamasa tunayopata lakini tunakatishwa tamaa na matokeo ya kazi hiyo. Tatizo tunatafuta heshima yetu kwa kulinganisha kiasi gani cha mali ulichonacho, mafanikio ya nje na watu ambao unaambatana nao. Hali ya maisha ni kwamba kuna wakati mambo hayaendi kama tulivyotarajia, au hatujapata mali kama tulivyodhani lakini haimaanishi kwamba heshina yetu imeondoka la hasha. Endelea kujiehshimu na utaheshimika kadri siku zinavyoendelea.
6. Heshimu watu wengine
Kama huheshimu watu wengine, unategemeaje kupata heshima? Heshina ni kuwa na ujasiri wa ndani na uhakika wa wewe ni nani lakini huu sio ujasiri wa kujiona kwamba uko juu ya watu wengine. Kama tutajisikia furaha kwamba heshima ni kujiona uko juu na watu wanaokuzunguka ukawaona wako chini yako, hapo umepotea inakubidi kwanza upya namna ya kuheshimu utu wa mtu mwingine ndipo utaweza kuheshimika. Kama utaweza kuangalia na kukumbuka uzuri wa tabia ya mtu ni rahisi sana kukumbuka tabia yako nzuri.
7. Usijichukie kamwe
Huwa tunafanya makosa, tunaweza kuwa tumefanya makosa lakini haitakiwi ukajiona hufai kwasababu ya kosa ulilofanya na kwanza kujichukia. Hutakiwi kufanya hivyo ni kujiharibu mwenyewe.

8. Samehe
Wasamehe wengine na ujisamehe mwenyewe. Usiishi kutokana na yaliyotokea hapo kabla na kujiweka kwenye mazingira magumu. Kama akili yako imejawa na makosa ya hapo kabla utajiona mkosaji wakati wote na utashindwa kujithamini. Usiruhusu hali hiyo ikateka maisha yako.
9. Usitegemee sifa za watu
Kama kujiheshimu kwako na utu wako unategemea watu wengine basi hilo ni tatizo. Sifa za watu huwafanya watu wengi kulewa na uishi maisha yasiyo ya kwao. Heshima yako inabidi uwe huru kutoka kwako mwenyewe na isitegemee sifa za watu wengine.
Je unajengaje heshima yako binafsi? Je unajengaje heshima yako binafsi? Reviewed by WANGOFIRA on 07:35:00 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.