Ilani ya vyama vya ADC, ACT sasa hadharani


Mgombea Urais kwa tiketi ya chama cha Alliance
Mgombea Urais kwa tiketi ya chama cha Alliance for Democratic Change (ADC), Chief Lutasola Yemba (katikati) akiwa ameshikana mikono na mgombea mwenza, Said Miraji (kulia), na Mgombe Urais wa Zanzibar kupitia chama hicho, Hamad Rashid Mohamed baada ya kupitishwa na wajumbe wa mkutano mkuu wa chama hicho uliofanyika Dar es Salaam jana. Na Mpigapicha Wetu 
Dar es Salaam. Wakati joto la Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25, mwaka huu likiendelea kupanda, vyama viwili vya ACT-Wazalendo na ADC ndivyo vilivyokamilisha ilani zake na kutangaza kwa umma, huku viongozi wa vyama vingine wakitangaza kukamilisha kazi hiyo kabla ya kuanza kampeni.
Kitabu hicho cha ilani kwa kila chama, hubeba ahadi za kuwatumikia wananchi.
Vyama vya UDP, PPT-Maendeleo, Sau na CCK, jana walisema watakachokifanya kwa sasa ni kuboresha ilani zao kwa ajili ya uchaguzi.
Katibu Mkuu wa Sau, Ali Kaniki alisema wameshanza kufanya maboresho ya ilani yao kwa baadhi ya vipengele.
Mwenyekiti wa UDP, Mkoa wa Dar es Salaam na mjumbe wa kamati kuu ya chama hicho, Joackim Mwakitinga alisema sehemu ya ajenda katika kikao cha ndani cha Agosti 15, mwaka huu ni kupiti ilani ya chama.
Mwenyekiti wa UPDP, Fahmi Nasoro Dovutwa alisema chama kinaendelea na maandalizi ya kupitia ilani ya chama hicho.
Katibu Mkuu wa CCK, Renatus Muhabi alisema ilani ni sehemu ya ajenda katika vikao vya kamati kuu ya chama hicho vitakavyoanza leo, ili kupitisha jina la mgombea urais, ubunge na udiwani.
Kiongozi Mkuu wa ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe alijinadi akisema chama chao ndicho pekee kilichokamilisha kuandaa ilani.
Mwenyekiti wa APPT-Maendeleo, Peter Mziray alisema tangu mwaka 2005, chama hicho kimekuwa kikifanyia maboresho ya ilani yake.
Kwa upande wa Mwenyekiti wa DP, Mchungaji Christopher Mtikila alisema hakutakuwa na mabadiliko makubwa katika ilani ya mwaka huu kutokana na ubora wake.
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe hivi karibuni, alibainisha kuwa ajenda ya kuandaa ilani itakasimishwa kutoka mkutano mkuu kwenda kamati kuu, ambayo itaanza vikao leo.
Msemaji wa Chadema, Tumaini Makene alisema jana kuwa baada ya kukamilika kwa ilani hiyo, itapitiwa na vyama vingine vinavyounda Ukawa ili kuijadili kabla ya kuitangaza rasmi kwa umma.
“Hiyo ndiyo itakuwa ilani ya Ukawa baada ya kupitiwa na chama na baadaye vyama vingine ndani ya Ukawa,” alisema Makene na kuongeza:.
“Kwa sababu tumeamua kuungana kwenye uchaguzi huu, basi kile tunachokusudia kufanya lazima tuwape na wenzetu wapitie kisha ndipo nasi tutangaze kwa umma.
Mwenyekiti wa CCM, Jakaya Kikwete hivi karibuni alisema halmashauri kuu ya chama hicho itabeba jukumu la kushughulikia maandalizi ya ilani.

Ilani ya vyama vya ADC, ACT sasa hadharani Ilani ya vyama vya ADC, ACT sasa hadharani Reviewed by WANGOFIRA on 01:34:00 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.