IJUE ZANZIBAR NA UTALII WAKE
Na, baraka Ngofira
0763580901
0763580901
Mji mkongwe wa Zanzibar ni mji wenye historia kubwa na jina
kubwa sana hasa kwa kusifika katika biashara ya utumwa ambapo kulikuwa na soko
kuu la Afrika Mashariki la kuuzia watumwa kutoka katika nchi zinazozunguka
Afrika ya mashariki.
Historia haiishii
kutaja tu kama mji huu ni maarufu katika uuzaji na usafirishaji wa watumwa bali
pia mji huu unasifika kwa kuwa na watu wengi maarufu ambao kusahaulika katika
historia ya dunia ni vigumu kama vile sultan Seyyid Said, Tippu Tip, Siti binti
Said ambaye alivuma kwa uimbaji wa taarabu za Kiswahili, pia wapo Shekh
Abdallah saleh Farsy ambaye ni mwandishi wa vitabu maarufu na mtafsiri wa Quran
katika lugha ya Kiswahili.
Mji huu mkongwe wa Zanzibar sio tu unasifika kwa historia
ndefu bali pia ni mji ambao umeingizwa kwenye urithi wa dunia ukiwa na fukwe
nzuri za kuvutia, maboma ya kuvutia na yaliyojaa maajabu ikiwemo jumba
linalofahamika kama Beit-al-ajaib katika lugha ya kiarabu umaajabu wa jumba ili
ni kuwa na nguzo 44 zilizojengwa kwa
umahiri na umaridadi na uimara wa hali ya juu.
Jambo la kufurahisha na kuvutia katika jingo hili ndilo
jengo la kwanza Afrika Mashariki na kusini mwa jangwa la sahara kuwa na umeme
na lifti, na hivyo kulifanya kuwa jumba la kitalii linalovutia watalii na watu
wengine wafikao Zanzibar kwenda kutalii na kutazama jengo hili.
Pia limekuwa kivutio kikubwa kwa watalii kuja kujifunza tamaduni
na mambo ya kale na hatua mbalimbali za kimaendeleo zilizo kuwa zikifanyika
Zanzibar kwa kale na zinazo endelea mpaka sasa, kwa kweli ufikapo Zanzibar
usisite kutembelea kwenye jengo hili la kimaajabu.
Kivutio kingine kinachovutia watu kwenda kutalii Zanzibar ni
mji mkongwe wa Zanzibar mji wenye historia kubwa na jina kubwa duniani , mji
uliokaliwa na watu wengi, mji wenye majumba mengi ya kitalii , makanisa na
misikiti ya kihistiroria yote yanapatikana kwenye mji mkongwe wa Zanzibar.
Nyangumi nao wamekuwa kivutio kikubwa hasa kwa watalii
watokao bara na nchi nyingine kuja kupiga picha nyangumi wanaoruka na kuonekana
kwa uzuri wakitokea majini na kisha kutumbukia majini. Nyangumi hawa
wamewavutia maelfu ya watalii kutembelea Zanzibar na kujionea kwa macho yao na
wwengine kubaki midomo wazi wakiwashaa nyangumi hawa jinsi warukavyo na
kutumbukia majini, kwa kweli Mungu aliumba ndiyo maneno ambayo uwatoka mara
nyingi watu hawa.
Ukiachilia mbali nyangumi uwepo wa fukwe nzuri za kuogelea
na kupumuzikia za Kendwa,Mungwi,na kiwengwa ni fukwe nzuri za kuvutia
zinazokusanya watu wengi hususani nyakati za jioni na nyakati za sikukuu kama
vile za Maulid na zile za Xmass na mwaka mpya . sio tu ni fukwe nzuri pia zina
upepo mwanana unaowavutia watu wapate fursa hii hadhimu ya kukaa na wale
wawapendao na muda mwingi kubadilisha mawazo.
Pia magofu ya kihistoria , chochoro nazo ni vivutio vikubwa
hasa kwa wilaya ya mjini Magharibi ambapo watarii hutumia fursa hii adhimu
kutembelea na kushuhudia majengo haya na magofu yaliyojengwa kwa umahili na
umaridada na mpaka leo yanahifadhiwa vizuri ili kuendelea kuwavutia watu wote
wanaotembelea Zanzibar.
Pia uwepo wa Kima wekundu wanaopatikana kwenye misitu ya
Jozani na Ngenzi nao wamekuwa kivutio kikubwa sana hasa kwa watalii wanaofika
kutembelea katika misitu hii ya ajabu kujionea wanyama hawa ambao ni adhimu
kupatikana bara na katika misitu mingine iliyopo bara na katika nchi nyingine
duniani. Kweli maajabu ya kima hawa na rangi zao zimekuwa kivutio kikubwa sana.
Uwaangaliapo na hata kupiga picha za kwenda kuonesha watu ambao hawajawahi
kuwaaona kima hawa na maajabu yao.
IJUE ZANZIBAR NA UTALII WAKE
Reviewed by WANGOFIRA
on
07:58:00
Rating:
No comments: